Uhamisho

Yanga yamsajili beki wa Simba

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imeendelea na usajili wake wa kimyakimya na mapema kama mwalim Mwinyi Zahera alivyosema huku wakifanikiwa kumsajili beki wa kati wa Simba.

Yanga imesaini Lamine Moro raia wa Ghana akitokea klabu ya Buildcom nchini Zambia kwa mkataba wa miaka miwili. Beki huyo mwenye miaka 25 huku akiwa na mwili mkubwa akimudu vizuri kucheza nafasi ya ulinzi.

Lamine Moro (mwenye jezi nyekundu) katikati akipiga mpira mbele ya mchezaji wa Afc Leopard

Ikumbukwe Lamine Moro aliletwa nchini na klabu ya Simba kwa mara ya kwanza wakiwa na nia ya kumsajili. Moro alivaa jezi ya Simba katika michuano ya Sportpesa Supercup akifanyiwa majaribio na benchi la ufundi la Simba.

Kupitia mtandao wao wa kijamii Yanga wamethibitisha kumsajili Lamine Moro. Huku pia wakitarajiwa kuendelea kushusha majembe mengine.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.