Rais wa Yanga Hersi Said (kulia) akiwa na Makamo wa Rais Arafat Hajji.
Tetesi

Yanga Yataja Sababu za Kusajili Nyota Afrika Kusini

Sambaza....

Yanga walikuwa nchini Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wakicheza na Marumo Gallants na hawakuondoka hivihivi tuu bali huenda wakarudi na nyota kutoka huko. 

Yanga waliotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na kujihakikishia tena nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika wamemtupia jicho fowadi wa Afrika Kusini, na Rais wa Yanga Hersi Said ameeleza nia yao. “Lengo kuu ni katika sehemu ya mpira wa miguu. Tunahitaji mchezaji ambaye anaweza kutupa matokeo uwanjani, pili, pia ni ushirikiano wa mashabiki ili kuunda PR nzuri kwa klabu nje ya nchi,” aliiambia FARPost na kuongeza “Nimepata wachezaji kutoka nchi mbalimbali Kongo, na tukienda Kongo sasa Yanga ikiwa inacheza, ni kama Yanga iko nyumbani kwa sababu tuna wachezaji kutoka huko.

“Wakongo wanaisapoti timu. Vivyo hivyo kwa Burundi. Vivyo hivyo kwa Uganda. Nina mchezaji wa Uganda, Khalid Aucho, na sapoti kutoka Uganda ni kubwa kwa Yanga. “Pia tumepata Mburkinabe – Stephane Aziz Ki; Tumepata mchezaji kutoka Ghana, Mali Diarra. Wachezaji hawa wana msaada mkubwa kutoka kwa nchi zao.

Rango Chivaviro anahusishwa na Wananchi Yanga

“Tulienda kucheza na Real Bamako nchini Mali, na idadi ya wafuasi waliokuja kuunga mkono Young Africans ilikuwa sawa na mashabiki wa nyumbani. Ni kwa sababu Diarra anatoka Stade Malien na tulikuwa tunacheza Real Bamako. Kwa hivyo wafuasi wa Stade Malien waligeuzwa kuwa wafuasi wa Young Africans.

“Hali hiyo hiyo tunaitarajia  ikiwa tutasajili mchezaji wa Afrika Kusini. Kwa hakika tutakuwa na idadi kubwa ya mashabiki kutoka Afrika Kusini kumsapoti mmoja wao. Kwa hivyo, ndio, sababu za kwanza ni za kimpira wa miguu, na nambari ya pili ni ushiriki wa mashabiki na kuunda uhusiano kati ya kilabu na wafuasi nje ya nchi.”

Yanga ni moja ya klabu zinazohusishwa na mshambuliaji wa Marumo Gallants, Ranga Chivaviro. Na Hersi Said alipoulizwa kama ndiye aliyelengwa, Said alisema: “Hakuna maoni katika hilo”.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.