Sambaza....

Zikiwa zimebakia takribani siku mbili tu kwa Stars kucheza na Uganda jijini Kampala  beki wa kati wa klabu ya Yanga na Taifa Stars, Kelvin Yondani ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kufuatia kupatwa na majeraha ya mguu.

Kelvin Yondani sasa ataukosa mchezo huo muhimu wa kuwania kufuzu Afcon nchini Cameroon. Mchezaji huyo ameumia mguu na kwa mujibu wa daktari wa timu ameshauri ni vema akasalia nchini kwa ajili ya matibabu zaidi.
Wakati huo kikosi cha Stars kinaondoka leo mchana kuelekea nchini Uganda.

Stars sasa imebaki ikiwategemea Abdi Banda, Agrey Morris na David Mwantika katika eneo la ulinzi wa kati. Huku Kelvin Yondani akiacha pengo kutokana na uzoefu mkubwa aliokua nao katika mechi za Kimataifa.

Sambaza....