Zana
Blog

Zana ajiunga na AS Vita Club.

Sambaza kwa marafiki....

Mchezaji wa Zamani wa klabu ya Simba, Zana Oumary Coulibaly leo amejiunga rasmi na klabu ya AS Club Vita ya Kinshansa nchini Congo kwa mkataba ambao bado haujawekwa wazi.

Zana ambaye aliitumikia Simba kwa nusu Msimu amepata dili hilo baada ya kutemwa na wekundu hao wa Msimbazi kutokana na kushindwa kuvaa viatu vya Shomari Kapombe kisawasawa baada ya kupata majeraha kati kati ya msimu.

Zana atakumbukwa zaidi na jamii ya wana Simba kutokana na muonekano wake wa kipekee, ukaribu na mashabiki , vituko na aina ya uchezaji wake wa kupiga krosi yaani kumwaga maji na yakamwagika.

Kandanda inamtakia kila la heri, Zana Coulibaly katika changamoto yake mpya.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.