Kipindi haya yote yanatokea, kumbe Msimamo wa TFF ulikuwa na kasoro, Kumbe Kagera Sugar ilibidi ndio wakacheze Playoff na Stand United Washuke daraja jumla jumla…Tff bhana we acha tu.
Viwanja vya Afrika huwa havina watazamaji wengi kiasi cha kuwatisha wageni. Yanga imezoea kucheza viwanja vya ugenini vyenye mashabiki waliojaa mpaka pomoni ligi kuu, hivyo si rahisi kutishwa na idadi kiduchu wa mashabiki wa Rollers.
Kandanda haijakuacha nyuma pia, kama ilivyo utaratibu wetu tutaendelea kukuletea ratiba, matokeo bila kusahau wafungaji bora wa kila mwezi wa Ligi Kuu.
Yanga imeweka kambi Morogoro, ikijiandaa na mechi za Ligi kuu na Mabingwa wa Afrika, pamoja na maandalizi ya Wiki ya Mwananchi ambalo linalenga kuitaambulisha timu kwa wananchi.