Ligi Kuu

Auseems: Tunamkosa beki wetu muhimu leo

Sambaza kwa marafiki....

Simba leo inaendeleza zoezi lake la kula viporo katiki Ligi Kuu Bara ikishuka dimbani dhidi ya Allince School ya Mwanza katika dimba la CCM Kirumba.

Baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Kagera Simba sasa itajiuliza mbele ya Allince ambapo mchezo unatarajiwa kuwa mzuri na wakuvutia.

Habari mbaya kwa mashabiki wa Simba ni kukosa huduma ya beki wao mkongwe Erasto Nyoni kutokana na kuumwa.
Kocha wa Simba Patrick Aussems amethibitisha kukosa huduma ya beki wake huyo.

Chanzo kilieleza ” Kocha Patrick Auseems amethibitisha tutakosa Erasto Nyoni katika mchezo wa leo kutokana na kuugua. Wachezaji wengine watakaokosekana ni Pascàl Wawa na Shomary Kapombe”.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.