Sambaza....

Baada ya gumzo kuzuka sana mitandaoni na baadhi ya vyombo ya habari, ikiwemo tovuti yetu, kuhusu suala la Mpira wa Kitenge, hiki ndicho tovuti ya kandanda imefanikiwa kupata kutokana na udadisi wake.

Inasemekana mipira iliyochezewa  wakati wa mechi kati ya Yanga na Stand United (Yanga ikiiubuka kwa ushindi wa bao 4-3), haikuwa ya Ligi Kuu, bali ilikuwa ni ya CAF ambayo huwa haitolewi maana hutumika pia kwa Timu ya Taifa.

Tazama Mpira aliokuwa akikabidhiwa

Alex Kitenge, mshambuliaji alieyefunga Hat-trick ya kwanza Ligi Kuu msimu wa 2018/2019, alipewa taarifa kuhusu suala hili mbele ya kocha msaidizi, Athuman Bilal, kuwa atapatiwa mpira kutoka katika mipira ya Ligi na walitakiwa kwenda kuchukua kesho yake (Baada ya siku ya Mechi).

Huu ndio uhalisia juu ya kisa cha la Kinara wa mabao kabla za mechi za leo, Alex Kitenge na Mpira wake wa Hat-Trick thidi ya Yanga.

 

Sambaza....