Ligi Kuu

Ajib apewa kazi maalum ya kuandika historia leo!

Sambaza....

Mshambuliaji mtaalamu wa klabu ya Simba Ibrahim Ajib Migomba “Ibra Cadabra” leo ataanza katika kikosi cha Simba baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali katika timu.

Ajib amepewa kazi maalum ya kusaidiana na Meddie Kagere katika eneo la ushambuliaji la Simba mbele ya Wajelajela Tanzania Prisons ambao wanasifika kwa soka la kutumia nguvu haswa.

Endapo Simba itapa ishindi ama itapata sare leo itatawadhwa mabingwa wapya kwa msimu wa 2019/2020, huku wakiwa wameuchukua ubingwa huo kwa mara tatu mfululizo.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

1. Aishi Manula

2. Haruna Shamte

3. Gadiel Michael

4. Erasto Nyoni

5. Kennedy Juma

6. Gerson Fraga

7. Hassan Dilunga

8. Mzamiru Yassin

9. Medie Kagere

10. Ibrahim Hajibu

11. Miraji Athumani

Wachezaji wa akiba ni  Mlinda mlango Ally Salim,  Mohamed Hussein,  Pascal Wawa, Said Hamis,  Clatous Chama, John Bocco, Luis Miquissone.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.