Tetesi

Ajib huyoo TP-Mazembe!

Sambaza....

Kiungo mtaalamu “technician” wa Yanga sc Ibrahim Ajib Migomba ni kama anaendeleza wimbi la wachezaji wa Tanzania kufungua mipaka na kutoka nje ya nchi kujaribu bahati yao.

Klabu ya TP-Mazembe imeonyesha kutaka kujua kutoka Yanga kama ni kweli anamaliza mkataba na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Bara.

Barua ya TP Mazembe ipo hivi:

Ikumbukwe katika usajili wa msimu uliopita Tp-Mazembe walikua wakimnyemelea Ajib lakini ikaonekana wameshindwa kuafikiana katika dau . Hivyo sasa TP wamerudi mara ha pili na sasa hivi akiwa mchezaji huru na hii ni baada ya Ajib kumaliza mkataba na Yanga June mwaka huu.

Hivyo basi Tp Mazembe watampata Ajib Migomba bure kabisa bila klabu yake ya Yanga kunufaika chochote.

Kama atajiunga na TP- Mazembe Ajibu atakua amefuaya nyayo za Mbwana Samata aliepo Genk kwasasa na Thomas Ulimwengu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.