Ligi Kuu

Azam fc yaitibulia Simba

Sambaza....

Klabu ya Azam fc imefanikiwa kutoka sare na Simba sc katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam ukiwa ni mwendelezo wa klabu ya soka ya Simba kula viporo vyake ligi ikielekea ukingoni.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Uhuru huku uwanja ukiwa na umejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea jijini Dar es salaam Azam fc wamefanikiwa kutoka sare ya bila kufungana na Simba na hivyo kuzidi kuwachelewesha Simba katika mbio zao za ubingwa.

Kosakosa za hapa na pale zilitokea kwa timu zote mbili huku Cleotus Chama na Emmanuel Okwi wakipoteza nafasi za kufunga a wazi. Kwa upande wa Azam Obrey Chirwa pia alikosa bao la wazi akiwa yeye na Manula ndani ya boksi.

Kwa matokeo yao sasa msimamo unasomeka hivi:

Msimamo wa Ligi Kuu Bara

#TimuPWDLGDPts
13829636293
23827562986
338211253375
438131691555
53814816250
638121313-849
73813916-148
838111512-1048
938121214-1248
1038111413-647

Kwa matokeo hayo sasa Simba sc inahitaji alama nane ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu huu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.