Ligi Kuu

Azam ya Ole Cheche ni balaa!

Sambaza....

Kasi ya Azam fc kwa sasa imeonekana ni hatari na ya kuipitia mbali baada ya leo tena kuendeleza ubabe mbele ya Kagera Sugar kwa mara ya pili mfululizo katika dimba la Nyamagana.

Katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara (TPL) Azam fc wakiwa nyumbani katika dimba la Nyamagana baada ya kuuchagua kama uwanja wao wa nyumbani baada ya ule wa Chamanzi kufungwa ili kupisha Afcon ya vijana waliwapa tabu Kagera Sugar na kufanikiwa kuwafunga mabao mawili kwa sifuri.

Alikua ni Frank Dumayo katika dakika ya 3 aliwatanguliza Azam fc kwa shuti kali baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Nicholaus Wadada. Lakini katika kipindi cha pili Donald Ngoma alihitimisha shughuli baada ya kufunga bao la pili kutokana na mkwaju wa penati baada ya Dumayo kuchezewa madhambi na kipa wa Kagera Sugar Jeremia Kisubi.

Kwa ushindi huo Azam inaendelea kukamata nafasi ya pili ikiwa chini ya Yanga yenye alama 67 huku wakiwa juu ya Simba kwa alama 62 na Simba wakibaki na alama 57.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.