Moja ya mikutano ambavyo timu inaweza kutangaza viingilio au utaratibu wa mapato yao. Pichani ni Haji Manara, Msemaji wa Simba SC.
Ligi

Baba yangu mzazi ana akili za muuza ubuyu -HAJI MANARA

Sambaza....

 

Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga tambo zinazidi kuwa nyingi ambapo Leo msemaji mkuu wa Simba amedai kuwa mashabiki wa Yanga wanapokutana akili zinakuwa moja.

“Wewe mchukue profesa yoyote wa chuo kikuu, mchukue profesa ambaye ni daktari bingwa ambaye ni shabiki wa Yanga afu waweke pamoja na shabiki wa Yanga ambaye ni muuza ubuyu , akili zao zinakuwa pamoja”

“Hata baba yangu huwa namuuliza, kuna wakati nikiwa nazungumza na baba yangu kwenye mambo mengine anaonekana ni Genius kweli, lakini linapokuja suala la Yanga U-genius wake unapotea”- alimalizia kwa kusema hivo , msemaji huyo alikuwa anahojiwa na kituo cha radio cha Wasafi Fm


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.