
Kiungo fundi raia wa Zambia Rally Bwalya baada ya kuachana na Simba na kutimka nchini kuelekea Afrika Kusini leo ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya.
Bwalya alicheza mchezo wa mwisho wa Simba dhidi ya KMC ambao pia ulitumika kumuanga nyota huyo maarufu kwa jina la *Left footer magician”.

Rally ametambulishwa rasmi na klabu ya Amazulu ya nchini Afrika Kusini hivyo msimu ujao atawatumikia Wazulu hao katika PSL Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini.
Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 akitokea Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu. Mpaka anaondoka Simba na kujiunga na Amazulu alikua amesalia na mwaka mmoja. Inadaiwa amesaini miaka miwili kuwatumikia Amazulu.
Unaweza soma hizi pia..
Tamu na chungu za dakika ya mwisho!
Ligi kwa ujumla ilikuwa ngumu na yeye kusisimua licha ya bingwa kupatikana mapema lakini kiwango cha ushindani kilikuwa kikubwa hadi dakika ya mwisho.
Hizi hapa mechi kali zakumalizia Ligi!
Binafsi hii ndiyo michezo mikubwa miwili ninayoiangalia kwa jicho la uoga kwa kuwa ina maamuzi na hatma ya timu. Fiston Mayele na George Mpole!?
Huyu ndiye mchezaji wangu wa msimu
Tuandikie jina lake na kwanini unadhani anastahili kuwa mchezaji bora wa msimu.
Kiungo wa Stars asajiliwa Ubelgiji!
Kiungo huyo amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu na sasa atakua akitonekana katika Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji maarufu kama Jupiter Pro League.