Larry Bwalya
Ligi Kuu

Bwalya: Bado nina deni na Simba!

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi Simba sc Larry Bwalya anasema anajiona mwenye kudaiwa na mashabiki wa klabu ya Simba kutokana na jinsi walivyompokea klabuni hapo.

Bwalya amejiunga na Simba akitokea kwao Zambia katika klabu ya Lusaka Dynamos, ambapo inasemekana Simba waliwapokonya wenzao Yanga tonge mdomoni kutokana na Yanga pia walimuweka kwenye mipango yao ya usajili katika msimu huu.

Larry Bwalya

Alizungumza na mtandao wa klabu ya Simba Larry anasema kila akiingia uwanjani hujiona mwenye deni na mashabiki wa Simba kutokana na imani yao kwake.

Larry Bwalya “Kila ninapoingia uwanjani najiona nina deni kubwa sababu Wanasimba wana imani kubwa na mimi, siwezi kuwaangusha nitahakikisha najituma kwa kila hali ili kuwafurahisha”

Bwalya hatokua na kazi rahisi katika kuanza katika kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na uwepo wa viungo wengine aliowakuta klabuni hapo. Katika eneo la kiungo Bwalya anakwenda kukutana na Ndemla, Mzamiru, Fraga na Chama.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.