Blog

CAF ya Ahmad Ahmad mikononi mwa FIFA

Sambaza kwa marafiki....

Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, amependekeza kuombwa kwa wataalamu kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu la Dunia (FIFA) kuja kukagua mambo yanayoendelea katika Shirikisho hilo, taarifa kutoka mtandao wa CAF imesema. Mapendekezo hayo yalifanywa katika kikao cha Kamati Kuu ya CAF kilichofanyika Juni 19 mwaka huu jijini Cairo.


CAF hivi karibuni imekumbwa na tuhuma mbalimbali zinazohusiana na masuala ya rushwa/ubadhilifu, tuhuma hizo zikimuhusisha Rais huyo ambaye anatokea katika kisiwa cha Madagascar.


Ahmad Ahmad

Mbali na ukaguzi huo, wataalamu kutoka FFA watasaidia pia katika Kuangalia hali ya sasa ya Shirikisho, kusimamia  kusimamia mabadiliko ambayo yatapelekea uendeshwaji wa shughuli za Shirikisho katika uwazi, tija na kuongeza viwango vingine ili kuboresha uendeshwaji wa shirikisho hilo.

Ombi hili lilipitishwa na kamati hiyo, na katika sehemu ya mchakato huo walikubaliana kwamba fifa na CAF kwa pamoja watafanya ukaguzi wa shirikisho na ripoti yake kutolewa. Hivyo basi, Katibu mkuu wa FIFA,Bi Fatma Samoura ataongoza jopo hilo maalumu kwaaji ya kazi hii.Kazi ya jopo hili itachukua miezi 6, kuanzia Agosti 1, 2019 hadi Januri 31,2020. Muda utaongezwa kama kuna uhitaji kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Bi Samoura, jopo lake litakuwa na wataalamu mbalimbali ambao watafanya kazi na Rais Ahmad pamoja na timu yake katika nyanja tofauti tofauti, ambazo ni:
– Kuangalia shughuli za usimamizi wa CAF, ikiwa pamoja na utawala na taratibu za kiuungozi.
– Kuangalia tija na uweledi katika uendeshwaji wa michuano/mashindano ya CAF.
– Kusimamia/saidia ukuwaji na maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanachama wote


Amr Fahmy (kushoto, katibu mkuu wa zamani CAF) na Ahmad Ahmad (Kulia)

Mapema mwaka huu Katibu Mkuu wa CAF aliondolewa katika nafasi yake baada ya kuaminika kuripoti tuhuma kuhusu Ahmad, ripoti zikisema pia Katibu Mkuu huyo alipeleka nakala za tuhuma hizo moja kwa Moja FIFA. Tuhuma hizo mbali na kuhusishwa mambo ya mikataba iliyovunjwa na kugaiwa makampuni mengine, pia inahusisha marais wa mashirikisho kupokea fedha ambazo inaonekana ilikuwa ni hongo.


Taarifa ya CAF imemalizia kwa kuelezea kazi hii itafanywa bega kwa bega kati ya FIFA na  CAF kwa lengo la kuwahudumia wanachama wake, kuleta umoja, uimara, uweledi na tija katika maendeleo ya mpira wa miguu Barani Afrika.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.