Abdi Banda
Blog

Chama la Banda hali tete Afrika Kusini

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya soka ya Baroka fc anayochezea Abdi Banda inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika ya Kusini imeendelea kubaki nafasi za chini katika Ligi hiyo maarufu kama PSL.
Baada ya sare ya mabao mawili kwa mawili Baroka fc waliyoipata dhidi ya Free State Stars sasa Baroka inashika nafasi ya 14 kwenye ligi inayoshirikisha timu 16, huku wakiwa na alama 25 wakibakisha michezo mitatu tu ili kumaliza Ligi

Maritzburg Utd ndio inayoburuza mkia ikiwa na alama 21 huku juu yao akiwa Chippa Utd wenye alama 24 wakifwatiwa na Baroka fc ya kina Abdi Banda wenye alama 25 huku wote wakicheza michezo 27.

Ligi Kuu Africa Kusini utaratibu wa kushuka daraja huwa ni timu inayoburuza mkia ndip hushuka moja kwa moja mpaka daraja la kwanza na anaefwatia atakaemaliza Ligi katika nafasi ya 15 hucheza “Playoff” na timu kutoka daraja la kwanza ili kupata timu itakayocheza Ligi Kuu msimu unaofuata.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.