Ligi Kuu

Dady: Tanzania Prisons walitumudu.

Sambaza....

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Alliance ya Jijini Mwanza, Gilbert  Dady amekitaja kipindi cha kwanza cha mchezo wao na Tanzania prisons kuwa kiguimu zaidi kuliko kipindi cha pili kutokana na maumbo ya wachezaji wa Tanzania Prisons kuwa makubwa na kuwazuia kucheza soka lao.

Amesema lengo lao lilikuwa kupata alama tatu katika mchezo huo ambao uliisha kwa sare ya 1-1 lakini kwa namna ambavyo Tanzania Prisons walikuwa wakicheza kutafuta sare na faida ya maumbo yao ndio maana walishindwa kupata alama tatu.

“Unajua kama umeaangalia vizuri maumbile ya wachezaji wetu na wa kwao hilo lilikuwa tatizo la kwanza, lakini la pili wale walikuwa wametengeneza mbinu yao daima wao walikuwa wengi kwa maana kwamba tulikuwa hatupati upenyo wa kupiga hilo ndilo lilikuwa tatizo,” amesema.

“Tulijaribu kutanua uwanja ili waweze kutoka na kuja pembeni lakini bado walikuwa wanafunga zile njia za sisi kupita kwa hiyo walitumudu tuseme kipindi cha kwanza, lakini tulipokwenda mapumziko tuliwaambia namna ya kucheza kwa possession kuanzia nyuma na kwa kiasi kidogo tuliwamudu licha ya kushindwa kupata bao,” ameongeza.

Alama moja ambayo Alliance waliyoipata dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Nyamagana imewafanya kufikisha alama 25 na kukalia nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wakati Tanzania Prisons wao wakiwa na alama 16 katika nafasi ya 19.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x