Sambaza....

Kuelekea mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kati Mashetani Wekundu Manchester united dhidi ya Sevilla ya Hispania nini tutegemee?

Baada ya kupata matokea mazuri dhidi ya mahasimu wao Liverpool weekend hii Manchester United ambao wanapewa nafasi kubwa kusonga hatua ya robo fainali lakini bado wanakibarua kigumu mbele ya Sevilla ambao wao si kama Manchester walipoteza mchezo wao wa wikendi katika Laliga dhidi ya Valencia kwa mabao mawili ya Rodrigo.

Ugumu Wa Game Ulipo

Wiki mbili zilizopita katika uwanja wa Estadio R. Sanchez Pizjuan, tulishuhudia mechi ya upande mmoja ambapo kwa umakini wa David Degea kuzuia michomo kadhaa kikiwepo kile kichwa cha Luis Muriel kuimeifanya leo tuiangalie kivingine hii mechi kwamaana kuna mengi ya kupigania.

Image result for sevilla vs man utd images

Habari njema kwa wapenzi wa Manchester kurudi kwa Zlatan Ibrahimovic na Anthony Martial ”AirFrance” huku wakisubiri hatma ya kiungo Paul Pogba. wakati kwa upane wa pili nao Sevilla watamkosa mchezaji wa zamani wa Manchester city Jesus Navas anayesumbuliwa na kifundo cha mguu.

Je Wajua?

Mechi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Sevilla kucheza mechi ya ushindani katika uwanja wa Old Trafford ukiachia ile mechi ya hisani ya Rio Ferdinand mwaka 2013 wakishinda bao 3-1.

 Manchester United ina rekodi mbaya dhidi ya timu za Hispania katika mechi takribani 51 United wameshinda mechi 13 tu ikiwepo ya hivi karibuni ya Europa dhidi ya Celta Vigo.

Image result for sevilla vs man utd images

Nani wa Kutazamwa?

Sanchez hapana, Rashford inawezekana ila United itamtegemea Sajenti Lukaku.  Man utd itamtegemea Lukaku kuwapatia ushindi katika mechi hii.  Lakini kwa upande wa Sevilla wapo vizuri na Man utd inatakiwa wamwangalie sana Pablo Sarabia kiungo huyu Mhispania amekuwa katika kiwango bora kabisa na amechangia mabao matano ya Sevilla katika mechi nane zilizopita kumfanya kuwa mmoja wa wafungaji bora kabisa. Pia Ever Banega ni mtu muhimu katika eneo la ushambuliaji la Sevilla.

Image result for sevilla vs man utd images

Ushindi Uko Wapi?

Haitakuwa kama mechi ya kwanza kwani mshindi lazima apatikane sevilla wakicheza kandanda safi la Kihispania watakutana English flowing football wenyewe wanauita mipira mirefu na mashambulizi ya kustukiza kutoka kwa Manchester united.

Kocha wa Sevilla Vincenzo Montela  anakibarua kizito mbele ya mbabe Jose Mourinho ambae yeye anajua hakuna matokeo mengine zaidi ya ushindi ndio ambayo yataifanya timu ya Manchester united kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.

Image result for sevilla vs man utd images

Wazee wa kubeti.

Karata yangu naitupa kwa vijana wa jiji la Manchester.   

 

Mchopy Shabani Nyaa.

Sambaza....