George Mpole
Ligi Kuu

George Mpole anaishi ndoto zetu!

Sambaza....

Naaam mpaka sasa katika mzunguko wa 24 wa Ligi Kuu ya NBC Yanga yupo kileleni na alama 60, alama 10 mbele ya anaeshika nafasi ya pili Simba Sc.

Kuna Namungo nafasi ya tatu wakiwa na alama 36 halafu kuna Geita Gold ya George Mpole nafasi ya nne wakiwa na alama 34. Hawa ndio wanaume wanaufuzia zile nafasi tatu zakuiwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa.

George Mpole akimtoka mlinzi wa Simba Joash Onyango.

Hapo nafasi ya nne kuna hao Geita Gold ambao wapo pale kwa juhudi binafsi za George Mpole na ndio maana utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa ni 1 kwao lakini yeye pekeake Mpole ana mabao 13.

Ndio kinara wa ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya NBC ni mzawa George Mpole akimuacha Fiston Mayele mwenye mabao 12 na Reliant Lusajo mwenye mabao 10.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara 2018/19.

Kwa miaka ya hivi karibuni wageni wamekua wakipokezana na kutawala tuzo ya ufungaji bora tangu enzi za Hamis Tambwe, wakaja kina Okwi na Kagere wa Simba kabla ya John Bocco kuzima utawala wao msimu uliopita kwa kutwaa ufungaji bora akiwa na mabao 16 na kuwaacha Cris Mugalu, Prince Dube na Meddie Kagere nyuma.

George Mpole ni kama anaishi ndoto zetu za kutamani kuzima utawala wa wachezaji wa kigeni katika ligi yetu haswa katika eneo la ufungaji. 

Sio tuu kwamba anafunga magoli lakini pia anafunga magoli yakuvutia na kusisimua kwa aina zote akiwa na uwezo wa kutumia kichwa na miguu yote miwili kama ambavyo video hapo juu inavyoonyesha.

Kila lakheri George Mpole mimi binafsi nakutakia kheri na uzima tele katika harakati zako za kuwania ufungaji bora ili kwa mara ya pili mfululizo tuzo ya ufungaji bora ibaki nyumbani. 

Sambaza....