Tetesi

GSM na Yanga wakosa hela ya kumsajili Mwamunyeto

Sambaza....

Uongozi wa timu ya Coastal Union umesema kwamba mchezaji Bakari Nondo Mwamnyeto ataendelea kuhudumu katika klabu hiyo msimu ujao kwa sababu wameshindwa kupata muafaka kamili na uongozi wa Yanga ambao wameonyesha nia ya kumsajili.
_
Mjumbe wa kamati ya utendaji ndani ya klabu hiyo Hussein Ally amesema kwamba Yanga ndio klabu pekee hadi sasa iliyofika kwenye uongozi wa klabu hiyo ili kukamilisha usajili wa Mwamnyeto lakini swala hilo limeshindikana baada ya mchezaji kukataa dau la klabu hiyo ambalo ni shilingi milioni sitini.


_
Ally amesema kwamba mchezaji husika anahitaji dau la shilingi milioni mia moja,jambo ambalo limeonekana kua gumu kwa Yanga.
_
Amesema kwamba wao kama Coastal Union swala hilo wameliacha kwa mchezaji mwenyewe licha ya kusalia na mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuhudumu kwenye klabu hiyo ya mkoani Tanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.