Ligi

Hakuna MU-BRAZIL mjinga, SIMBA yaitisha Yanga

Sambaza....

Baada ya Jana Yanga kushinda kwa goli moja kwa bila dhidi ya Prisons kwenye mechi iliyochezwa Iringa katika uwanja wa Samora , Leo hii Simba ilikuwa inasubiriwa kuwajibu Yanga.

Simba ilikuwa na mechi kwenye uwanja wa Uhuru dhidi ya KMC,  mechi ambayo imeisha kwa Simba kushinda kwa magoli mawili. Magoli ambayo yamefungwa na Deo Kanda pamoja na Mbrazili Gerson Fraga.

Kwa matokeo hayo yamewafanya Simba kuzidi kuwaacha Yanga kwa jumla ya alama kumi , Simba imefikisha alama 31 na Yanga wakiwa na alama 21 katika nafasi ya tatu na Simba wakishika nafasi ya pili .

Hali hii inaifanya Yanga kuona mlima mrefu kwa kuachwa alama nyingi na Simba huku wakielekea kwenye mechi ya watani wa Jadi wakiwa nyuma ya alama nyingi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.