Edna Lema akishangilia na wachezaji wake baada ya mchezo kumalizika.
Kombe la Dunia

Hakuna namna ni kupambana nao tuu!

Sambaza....

Droo ya makundi ya fainali ya kombe la Dunia kwa wanawake nchini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika nchini India Oktoba 2022 imefanyika

Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa fainali hizi kupitia timu yetu ya Serengeti Girls kufanikiwa kutuheshimisha kwa kufuzu michuano hii mikubwa duniani kwa Wanawake wa umri huo

Droo ya makundi iliyofanyika Zurich Uswiss ijumaa hii tarehe
24/O6/2022 umepanga kama 4 ya timu nne nene kama ifuatavyo:

Makundi ya Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17!

Tukiangalia kundi letu washindani wetu kiukweli wamepiga hatua katika soka la Wanawake ndani ya mataifa yao na hata ushahidi wa viwango vya FIFA unawalinda

France ni ya 3 kidunia inapokuja soka la Wanawake huku Canada wakishika nafasi ya 6 na Japan wao wapo kwenye nafasi ya 13 nasi tupo 151.

Na hata uwekezaji kwenye soka la Wanawake wenzetu wapo maili kadhaa mbele huku siye ndiyo kwanza tukiwa tumeanza safari hiyo.

Maendeleo ya soka la vijana ( Youth Development) ndiyo kwanza tunaashiria kuanza sasa anagalau kwa kuwa na Category hiyo ya U-17 tulipaswa kuwa na category nyingine kama U-15 ili kutengeneza muunganiko mzuri sana na hao

Nachoweza kusema tunaenda kama wageni kwa maana zote za kuwa na adabu na nidhamu ya hali ya juu ugenini.

Hii haina namna tena ni lazima tupambane kwa dhati kulinda heshima ya Taifa Leo ,ila kiukweli ni kundi gumu sana.

Mchezaji wa Serengeti Girls akiwatoka wachezaji wa Cameroon.

Najua wengi wanadhani muda bado upo kuweza kutengeneza timu kiufundi na kimbinu kutokana na levo ya mashindano hayo

Ila ukweli utabaki kuwa hakuna muda uliowahi kutosha kwenye soka ni vyema tukaanza kupambana kwa maandalizi ya kisayansi.

Kila laheri Bakar Shime na mwanadada shupavu Edna Lema nyie ndiyo kutosomea dira.

Sambaza....