Uhamisho

Hapa kwa Morrison tunaongea Kiswanglish?

Sambaza....

Wapwa: Kuna maswali najiuliza sipati majibu hadi nikajikuta nakumbuka wimbo wa Kiswanglish uliimbwa na Witness akiwa ma kundi la Wakilisha nyakati fulani,

Hasa eneo lile ” najiuliza hili swali sipati jibu makini Wabongo twaongea kiswa…” Leo Wanazuoni wapana wa fikra ( IQ) unisaidie Mpwa wenu nimekwama.

Tuanzie kwenye lugha ya picha hapo kwanini Eng Hersi na gumzo la jiji Morrison wamekutanisha viwiko?

Fikra zangu zinanituma ni badala ya kushikana kiganja kwa kiganja kama ilivyotamaduni ya kupeana mikono kama salamu au ishara ya muafaka. Lakini najiuliza ( kisa cha kwenye wimbo)ule kwanini hawakufanya taratibu ambazo tulizozizoea? Napata jibu athari za ugonjwa wa Corona ulibadilisha tamaduni mbalimbali za Mwanadamu.

Natoka hapo nakuja kwenye Connection ya Maradhi ya Corona duniani ,Nafika mbali najisemea moyoni “ile si ilikuwa katikati ya mwezi wa 3?”.

Nakumbuka Tamko la Serikali yetu juu ya kusimamisha shughuli za michezo ilikuwa 17 /03/20? Narudi najiuliza kama mkataba wa kwanza tuliambiwa ni January 15 kwanini katika picha hii hawakusalimia kwa kukutanisha viganja.

Au Eng na Morrison ni Wasela Fulani wana tamaduni za kusalimiana kisela ( Wazee wenzagu wa vijiweni wanafahamu zaidi ) au kirastafariani?.

Lakini Mimi naamini waligeana mikono hivyo kwa minajiri ya angalizo la Corona kwa maana hiyo jambo hili lilifanyika wakati wa Corona Ikiwa hivyo sita ,sita kusema huu ni mkataba wa pili wa Morrison katika uwepo wake Yanga.

Mwisho narudi tena kwenu Wanazuoni kuomba msaada ,Je Morrison anacopy ya mkataba huu tunaouona pichani au hana? Kama anayo Copy (Nakala) ya Mkataba najiuliza aliipata wapi? Kwenye Nakala aliyonayo yeye ina shahihi za pande mbili kama si tatu au nne kwa maana ya mashahid?.

Suala lipo kwenye Mamlaka husika ushauri wangu tusubiri filamu hii nzuri.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.