Uhamisho

Haruna Moshi “Boban” amerudi!

Sambaza....

Kiungo mtaalamu fundi wa mpira Haruna Moshi Shabani Mawela amerejea tena Ligi Kuu Bara baada ya kukosekana kwa nusu msimu tangu alipoachana na Yanga sc.

Haruna Moshi msimu uliopita alikua akiitumikia Yanga chini ya Mwalim Zahera kabla ya msimu kuisha na Yanga kuamua kuachana nae lakini sasa amerudi kivingine tena VPL.

Haruna Moshi Bobani wakati wa kupasha misuli katika mchezo wa hisani kati team kiba na team samata

Boban amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miezi sita huku akiwa na jukumu kubwa la kuinusuru timu hiyo isishuke daraja. Singida United ni miongoni mwa timu za chini kabisa katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikishika nafasi 20 ya  ikiwa na alama 7 tu.

Boban anakwenda kukutana na swahiba wake Athumani Idd Chuji ambae yeye tayari ameshajiunga na Singida Utd katika dirisha dogo la usajili.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.