Blog

Hesabu za Simba kutinga robo fainali kuna kaugumu fulani hivi…

Sambaza....

Katika msimamo wa kundi D Shirikisho Afrika; Simba wanapatikana katika nafasi ya 3 wakiwa na alama nne, Asec mimosas wanabuluza Mkia wakiwa na alama 3 pekee ikiwa ni tofauti ya alama Moja na Simba.

Kileleni wapo wababe wawili RS Berkane wenye alama 6 na US Gendarmarie yenye alama 4 katika nafasi ya kwanza nay a pili Mtawalia.

Kama Ulivyo Mgawanyiko huu ndivyo ilivyokuwa kwa mechi za Nyumbani na Ugenini. Timu zote nne zimecheza jumla ya michezo Mitatu, kila mmoja akimuonja Mpinzani wake lakini tofauti ni yupi alikuwa Nyumbani na yupi alikuwa Ugenini.

RS Berkane katika mechi 3, 2 Amechezea Nyumbani na azote ameshinda, Moja alikuwa Ugenini na akapoteza; US GendarMarie katika nafasi ya Pili, amecheza mechi mbili nyumbani, Ameshinda Moja na kutoa sare Moja, na Akapoteza moja Ugenini akakusanya alama 4. Wawili hawa ndio waliocheza mechi mbili za nyumbani na Moja ya Ugenini na wote tunawaona wanaongoza Kundi.

Simba katika nafasi ya Tatu amecheza mechi Moja Nyumbani, na mbili Ugenini; Ameshinda Moja, ametoia sare Moja na kufungwa Moja, amekusanya jumla ya alama, ASEC katika nafasi ya mwisho; wameshinda mechi Moja ya Nyumbani na kupoteza mechi mbili za Ugenini na kujikusanyia alama 3 pekee.

Dalili ya awali kabisa kwa kundi hili ni KIla mmoja kuonekana kuwa na uwezo wa kushinda kwake.

Kwa kutumia kanuni hii ya kila mmoja ashinde kwake basi Simba ndio timu itakayokuwa na faida Zaidi katika kundi kwani ina mechi mbili Nyumbani ikiwa ni sawa na Alama 6 na kufanya jumla kuwa na alama 10, Asec Mwenye alama Tatu naye akishinda zote za nyumbani atakuwa na alama 9, US GendarMarie wao wana mechi moja tu nyumbani hivyo wakishinda watakuwa na alama 7, RS Berkane nao wakishinda mechi Moja ya nyumbani watakuwa na alama 9 sawa na ASEC.

Kwa kigezo hiki; Simba itaungana na mmoja kati ya ASEC au RS Berkane kwenda hatua ya Robo fainali.
Hizi ni hesabu tu; hesabu ambazo sio lazima kwenda kama Inavyoonekana hapa, lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba; Simba Kwenda mechi 2 za Ugenini kisha ikarudi na alama Moja bado inafaida kubwa kwani Yupo ASEC ambaye hajakusanya hata alama Moja katika mechi zake mbili za Ugenini.

Kwa kigezo hiki Unaweza kusema kuwa; Kati ya timu zote NNe Simba ndio iliyopata matokeo mazuri Zaidi kwani tayari imejihakikishia alama Moja ya ugenini tofauti na timu zingine.

HESABU ZA KUFUZU ZIPOJE?

Ili Simba kujihakikishia kufuzu bila Tabu yoyote inatakiwa kushinda mechi 2 za Nyumbani dhidi ya RS Berkane Machi 13 na dhidi ya GendarMarie April 3 zote katika dimba la Mkapa. Swali la Msingi hapa ambalo linahitaji majibu ni je Simba ina nafasi gani ya kushinda mechi hizo?

Kazi yangu leo ni Kupima Nafasi ya Simba katika michezo hiyo kwa kuangalia Kiwango kilichopo na JInsi gani kinaweza kuleta matokeo tarajiwa; lakini pia Nitashauri ni kipi kifanyike ili mambo yawe Mwemwele mwemwele kama Tunavyoyataka yawe.

Ili kujua kama Simba itakuwa na Uwezo wa kufuzu ama La lazima kwanza Ujue hali ya KIkosi kuanzia Utimamu wa Wachezaji kimwili na Kiufundi. Afya ya Mwili na Ufundi ndio Vitu viwili vinavyoweza kuibeba Timu au kuiangusha timu.
Licha ya kuwa nyumbani kwa mechi mbili lakini Kupata matokeo Nyumbani sio kitu chepesi cha kuongea kwa Mdomo; ni kazi ngumu.

Acha tukaone hali ya Timu kwa Ujumla wake.

Ukiitazama Simba Katika michezo 12 iliyopita utabaini kuwa hii sio Simba yenye makali makubwa; Hii sio Simba ya kuiwekea dhamana; bado haina uhakika Wa Ushindi hata kama Mechi itakuwa nyumbani.

Simba ya Franco ni Simba ambayo inajengwa kila siku; na Ujenzi wake hadi sasa haujafikia kiwango cha Kuridhisha. Kwanini? Kuanzia katika mechi ya Mapinduzi hasa ile dhidi ya Mlandege baada ya sare ya kutofungana; Simba ilianza kupata matokeo kwa mbinde. Simba wlaifanikiwa kuchukua kikomhbe cha Mapinduzi lakini hata hivyo hawakuwa na makali ya Kutisha na kwa jInsi mechi ilivyokuwa bila shaka Hata Azam nao walikuwa na nafasi sawa ya kubeba.

Baada ya Mapinduzi Cup; Simba Ikapoteza mbele ya Mbeya City, kisha Ikatoa sare na Mtibwa Sugar; bAdo haijakaa sawa ikapoteza tena dhidi ya Kagera Sugar.

Simba ikaja kupoteza msongo kidogo kwa Kuifunga Dar City goli 6-0 ASFC, Kisha ikashinda kwa Mbinde mbele ya Tanzania Prisons, ikaja Ikashinda tena Kiuwembamba Zaidi dhidi ya Mbeya Kwanza; Katika mechi zote Ushindi wake ulikuwa goli 1-0
Mchezo wake wa Kwanza Shirikisho Afrika Ulikuwa dhidi ya ASEC Mimosas ya Coutedvour Nyumbani na Kuibuka na Ushindi wa goli 3-1.

Hadi dakika ya 78 ya Mchezo huo Ubao ulisoma 1-1; hata Mashambiki wenyewe walianza kukata tamaa, na hata Kuamini mechi itatoka sare au Simba kufungwa Kabisa kabla ya Kapombe na Banda kufunga Goli 2 ndani ya dakika 2.
Kiufundi kabisa; licha ya Simba kushinda, lakini ilizidiwa vitu vingi lakini pia ilikuwa na mapungufu kadha wa kadha ya kimbinu kutoka kwa Pablo.

Simba hiyo hiyo ikaenda kupata sare ya 1-1 kwa Gendarmarie kabla ya Kufungwa goli 2-0 na RS Berkane.Kwa Mfululizo wa Matokeo haya na JInsi Timu ilivyocheza kutoka mechi moja hadi nyingine ni jibu tosha kuwa Simba haina Uhatari Kimbinu; Namaanisha katika kuijenga Simba; Pablo bado hajamaliza Homework yake; na hii huifanya Simba kuwa na Matege mengi inapokutana na Timu iliyoiva Kimbinu.

Simba inatafunwa na Vitu Vikuu Vitatu hadi sasa!

Mbinu za Pablo.

Simba ya Pablo inahaha sana kupata beki wa kati mwenye Kasi, lakini pia beki Kiongozi. Timu inapo-press kuanzia juu; Onyango na Inonga hulazimika kupanda ili kupunguza gepu kati yao na Kiungo wa Ulinzi. Hii huacha uwazi mkubwa kati yao na golikipa, uwazi huu mara nyingi hutumiwa na Wapinzani kwa Kupiga mipira mirefu kudondokea hapa.


Kwa kuwa wote hawana kasi; hujikuta wakimkimiza Mshambuliaji wa Upinzani bila mafanikio. Nenda katazame goli la Mbeya City, Kagera Sugar na Asec Mimosas Utaelewa ninachokwambia.
Hapa Unahitaji mabeki wenye kasi lakini pia wenye uwezo mkubwa kujua mechi inataka nini na wao wanatakiwa kufanya nini?
Lakini pia kukosekana kwa Muendelezo kwa Mabeki wa pembeni; Tshabalala na Kapombe. Wawili hawa Siku hizi hawana muendelezo hasa eneo la Kulia. Ni kweli wame-set standard za Viwango vyao lakini Ukweli ni kwamba, Msimu bado hawajaonyesha cheche zao.

Simba ya Misimu Minne iliyopita iliendeshwa na Falsafa ya kumiliki Mpira kwa kupiga pasi fupi fupi zenye mchanganyiko na ndefu za ku-shitch kulia na kushoto. Falsafa hii ilikuwa ni rahisi kuingia kwa Wachezaji kwa sababu ya Ukongwe wa Falsafa yenyewe.

Chini ya Falsafa hii ya muda Mrefu timu ilikuwa Imeungana katika kila eneo; Timu ilikuwa na Uhakika wa ushindi dhidi ya timu yoyote ile hasa katika uwanja wake wa nyumbani bila kubadili Falsafa. Timu nzima iliamini kuwa, njia nzuri ya Kushambulia ni kuwa na Mpira kwanza; na ndicho ilichokifanya.
Simba ya Pablo inashambulia katika vipindi Vya Mpito pekee. Hii inamaanisha; Simba yake haina mpango wa Kumiliki Mpira, badi ina mpango wa Kushambulia kwa kushtukiza tu.
Katika hili Simba ya Pablo itachukua muda mwingi kuandaa mbinu za kucheza timu ikiwa haina Mpira yaani jinsi ya kumpokonya Adui; Kisha Mbinu ya kushambulia kwa haraka, punde baaada ya kuupora Mpira.


Na ndio maana Simba hii ina Press kuanzia Juu, lakini Pia ni lazima Ianze na Wachezaji wenye Kasi kubwa ya Mbio wakiwa na Mpira na wakiwa hawana Mpira.


Katika hili Pablo anakutana na Changamoto kubwa mbili; Kwanza Wachezaji wengi wamekaa na Timu kwa muda Mrefu; hivyo zile mbinu za Kumiliki Mpira bado zimewaganda; wagumu Kubadilika.
Pablo yeye anataka Mpira wa kasi, lakini Wachezaji wao wanataka Kupoza Mchezo; hapo ndipo hupishana. Pili Pablo hajafanya Usajili; hivyo hana wanachezaji wanao-fit kwenye mbinu zake. Kivipi?


Ukilitoa eneo la Goalkeeping; maeneo yote Simba yana matatizo ya Kiufundi na hayaendani na Falsafa ya Pablo ndani ya Simba.
Simba ya Pablo inahaha sana kupata beki wa kati mwenye Kasi, lakini pia beki Kiongozi. Timu inapo-press kuanzia juu; Onyango na Inonga hulazimika kupanda ili kupunguza gepu kati yao na Kiungo wa Ulinzi. Hii huacha uwazi mkubwa kati yao na golikipa, uwazi huu mara nyingi hutumiwa na Wapinzani kwa Kupiga mipira mirefu kudondokea hapa.


Kwa kuwa wote hawana kasi; hujikuta wakimkimiza Mshambuliaji wa Upinzani bila mafanikio. Nenda katazame goli la Mbeya City, Kagera Sugar na Asec Mimosas Utaelewa ninachokwambia.
Hapa Unahitaji mabeki wenye kasi lakini pia wenye uwezo mkubwa kujua mechi inataka nini na wao wanatakiwa kufanya nini?
Lakini pia kukosekana kwa Muendelezo kwa Mabeki wa pembeni; Tshabalala na Kapombe. Wawili hawa Siku hizi hawana muendelezo hasa eneo la Kulia. Ni kweli wame-set standard za Viwango vyao lakini Ukweli ni kwamba, Msimu bado hawajaonyesha cheche zao.

Kiungo wa Ulinzi.

High Pressing ya Pablo inahitaji kiungo wa Ulinzi mwenye sifa za Kiulinzi muda huo huo ana sifa za kiushambuliaji; ambapo kiuhalisia Pale Simba hayupo.


Mkude Ni mzuri akiwa na Mpira sio bila Mpira, lakini Pia Yuko Slow sana, Sio mbweha anacheza eneo dogo mno la uwanja; hivyo hawezi kuwa Kiunganishi cha maeneo ya pembeni na hawezi kusaidia Ulinzi.
Lwanga ni Mzuri akiwa hana Mpira, ni Mbovu akiwa na Mpira; hana Heatmap Kubwa, yuko Slow, Sio Mzuri wa Ku-press, hivyo bado ha fit kwenye mbinu hii.
Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Erasto Nyoni; Ni wazuri lakini hawana Muendelezo; lakini kubwa kupita yote ni kufanya mambo haya mawili nusu nusu bado hawajakamilika.
Udhaifu huu ndio humfanya Pablo kuanza na Viungo wa ulinzi wawili; kitu ambacho kwangu mimi naona ni kupunguza makali ya Timu katika kujenga mashambulizi.
Ukiachana na maeneo haya mawili; eneo linguine ni eneo la Ushambuliaji. Mugalu, Boko na Kagere wote hawana makali; kwenye nafasi 5 wanapata 1; Kiufupi wameshuka Viwango; lakini pia lazima nikiri kuwa Hali hii ni ya Mpito kwani Binafsi namkubali Mugalu bila Kumsahau kagere katika kusaidia Kukabia juu.

Jambo la Mwisho linaloitafuna Simba ni Majeruhi.

Kuwakosa wachezaji wane hadi 6 katika mechi moja tena wote wakiwa ni wa kikosi cha kwanza basi jua kabisa kocha lazima ahahe kuhakikisha watakaoaminiwa wanafanya kazi kubwa.


Hatari Zaidi ni kwamba, Hata wakirejea bado watahitaji tena MUda Mwingine wa ziada ili kurudi katika viwango vyao.

Je nini KIfanyike ili kupunguza athari hizi na kuipa Simba matokeo mazuri kufuzu Robo fainali?

Kwanza kabisa ni muda mzuri kwa sasa kuanza kuandaa saikolojia ya Timu nzima, hasa kuweka set-up za Upambanaji; Kila Mchezaji sharti aingiwe na roho kupambana kama ya Mnyama Simba.


Katika Mpira, Motivation ina nafasi kubwa sana kuliko hata unavyoweza kudhani; Motivation inaweza kuigeuza Ruvu shooting kuwa Barcelona, Motivation inaweza kumgeuza Sadio Kanoute kuwa Paul Pogba na Mzamiru Yassin kuwa Ngholo kante.
Hivyo Klabu kama klabu inapaswa pia kuwekeza nguvu zake hapa.
Binafsi naamini, Wachezaji wakishapandishwa Ari na wakapanda, Mzuka Ukaongezeka basi tarajia Vipigo Vitakatifu kwa yeyote atayetua kwa Mkapa.


Lakini lazima nikiri kuwa, mashabiki wana nguvu kubwa sana wakati wa dakika 90 kuhakikisha wana wamotivate wachezaji kwa kushangilia, lakini pia Kocha ana nafasi ya kurekebisha baadhi ya vitu kwani timu zote tayari ameshaziona na anajua wapi ni bora na wapi ni dhaifu.

Kwa leo acha niishie hapa; Wangapi tunaamini Simba itatoboa Robo Fainali?

Sambaza....