Wachezaji wa Simba wakishangilia mbele ya mashabiki wao
Ligi Kuu

Hii ndio tofauti ya Simba sc na wao!

Sambaza....

Ligi Kuu Bara imeendelea leo  kwa michezo 10 kupigwa huku timu zote zikishuka uwanjani kutafuta alama tatu, huku vita kubwa ikiwa ni katika kushuka daraja na kugombania ubingwa.

Simba sc, Azam fc na Yanga sc wao wanabanana katika nafasi za juu ili kutafuta kuunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Bara lakini huku chini kuna Ndanda, Singida, KMC, Biashara utd, Mbeya city, Mbao fc na Mwadui zikipambana kutokushuka Ligi daraja la kwanza.

Huku kwenye vita ya ubingwa inaonekana vita hii haina muda mrefu kwa maana kua Azam fc na Yanga wanaonekana wakitaka kufupisha mbio hizo kwa kuiruhusu Simba kunyakua ubingwa mapema.

 

Mpaka sasa Simba anaongoza Ligi akiwa na alama 56 akiwa na michezo 22, wakati Azam anashika nafasi ya pili akiwa na alama 44 na michezo 22 halafu anakuja Yanga akiwa na alama 39 na michezo 20. Maana yake Simba anaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 12 na Azam fc anaemfwatia wapili.

Katika michezo ya leo ya raundi ya 22 Simba, Azam fc na Yanga zote zimeshuka dimbani leo, lakini ni Simba pekee ndie alieibuka na ushindi tena ugenini dhidi ya Lipuli ya Iringa.

Wakati ukitegemea Azam fc na Yanga zipate ushindi ili kuendelea kumpa presha Simba anaeongoza lakini sivyo. Azam na Yanga wanadondosha alama tena wakiwa katika uwanja wa nyumbani. Halafu upande wa pili Simba iliyoko ugenini inakusanya alama tatu katika uwanja mgumu na timu ngumu ya Lipuli fc.

Kiungo wa Coastal Union Issa Abushehe akimiliki mpira mbele ya mlinzi Nicholaus Wadada wa Azam fc

Na hapa ndio unaona tofauti ya Simba na wapinzani wake katika mbio za ubingwa. Simba nakwenda kubeba alama tatu kibabe ugenini, lakini Azam fc anakubali kufungwa nyumbani na Coastal Union halafu Yanga sc anadondosha alama mbili kizembe kwa kukubali suluhu katika uwanja wa Taifa dhidi ya Tanzania Prisons.

Azam fc na Yanga wasipoamua hii Ligi ya ubingwa wataimaliza mapema sana na kutuachia ligi ya kushuka daraja maana kwa mwenendo huu Simba huenda akakabidhiwa ubibngwa mapema kama ataendelea na mwenendo huu wa kukusanya alama haswa katika viwanja vigumu tena mbele ya timu ngumu.

Sambaza....