Uhamisho

Huyu Okrah mtakula maneno yenu!

Sambaza....

Wapwaa, balaa la fundi huyu hakika kwa Okrah Simba wamelamba dume ashindwe tu mwenyewe kucheza ila ni bonge la mchezaji.
Nimebahatika kumuona akicheza mechi kadhaa za ligi na vikombe vingine pale nchini Ghana naomba niseme Okrah ni fundi.

Kama ‘atapata’ mapokezi mazuri ndani ya Simba toka kwa wenzake basi timu zinazokutana naye kazi wanayo.

Ubora wake uko wapi basi?
1- Anacheza nafasi zote za mstari wa mbele ila mtamu kama si ‘mcharo’ kwenye kiungo mshambuliaji (attacking midfielder) lakini si haba kwenye winga zote mbili kulia na kushoto.

Augustine Okrah.

2 Mwendo (Pace) hapa ndiyo italimwa na kupaliliwa jamaa kajaliwa kasi ya hali ya juu kama unapita kwenye page yangu ya instagram kwa handle ya @tiganatz majuzi nilipost mchezaji wa Kibrazil mwenye zaidi ya kasi ya binadamu wa kawaida akiwapiga chenga wenzake nikatania nje ya kazi ya soka angafanya jukumu gani jingine wengi wakajibu kuwa kibaka.

Mwanaume huyu inapokuja swala la kasi kufanya maamuzi kwa wakati basi ndiyo pahala pake nakumbuka siku ya kwanza namtizama pale Accra Stadium nilijiuliza bado yupo Africa? Kwanini hayupo Ulaya?.

Matumizi mazuri ya miguu yote kwa ufasaha mkubwa hapo ndiyo imelala huwezi kujua upi ni mguu wake dhaifu na upi ndio anautumia kitu ambacho ni silaha muhimu kwa mchezaji hasa wa kariba ya Kimataifa.

Agustine Okrah mchezaji mpya wa Simba Sc.

Nguvu za miguu, ni mzuri sana sana kupiga kwa mbali na ana shabaha. Amekuwa na uwezo mkubwa wakufunga na ndio maana haishangazi kuona ana goli 14 katika michezo 31 toka idara ya kiungo.

Silaha yake nyingine ni uwezo wa kufufua mipira ‘iliyofariki’ (free kick taker) jamaa ni hodari sana inapokuja jambo hilo huenda kwenye eneo hilo akawapa changamoto vizuri Never Tigere na David Luhende ambao kwa kwa ligi yetu ya NBC ndiyo hatari 

Kwa kasi yake na utundu wa makocha wanaweza kumtumia vizuri kwenye mashambulizi ya kushtukiza na magoli yake mengi ni ya mfumo huo kwa maana hiyo makipa mchukue taadhari huyu jamaa hanaga kujiandaa sana.

Ukitazama video zake kama ambavyo zimesambaa mitandaoni utaakisi hili ninachokisema na kusadiki ni aina gani ya mchezaji ambae Simba imemsajili. 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.