Uhamisho

Ihefu yanasa mshambuliaji Azam na beki wa Simba!

Sambaza....

Matajiri wa mchele Ihefu Fc wameendelea na kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC kwa kunasa wachezaji wazoefu na waliopitia vilabu vikubwa nchini.

Baada ya kupanda Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2020/2021 na kushuka wamepata somo na sasa wameamua kuingia sokoni kusajili wachezaji wazoefu.

Obrey Chola Chirwa.

Ihefu Fc chini ya Zubery Katwila imefanikisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa AzamFc na Yanga Obrey Cholla Chirwa aliekua anaitumikia Namungo msimu uliomalizika.

Si tu Obrey Chirwa lakini pia wamefanikiwa kupata saini ya Juma Said Nyosso “Koulibaly” mchezaji wa zamani wa Simba, Kagera Sugar na Mbeya City ambae alimaliza msimu akiwa na matajiri wa dhahabu Geita Gold.

Juma Said Nyosso.

Nyota wote hao wawili wanakwenda kuongeza nguvu katika kikosi cha Ihefu mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliomalizika. 

Juma Nyosso na Obrey Chirwa wanakwenda kuungana na kina Raphael Daud, Joseph Mahundi na Mwasapili ambao wao walikuwa na timu tangu ipo Ligi ya Championship.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.