EPL

Je wajua, Arsenal imepata ushindi katika michezo 6 tu ya EPL?

Sambaza....

Arsenal “The Guners” imekua na mwenendo mbaya katika Ligi huku ikipelekea kupanda ushindi kiduchu katika Ligi. Katika EPL msimu huu mpaka sasa imekua na kiwango cha kusuasua huku pia ikiwa na uwiano mbovu wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Mpaka sasa Arsenal imepata ushindi katika michezo sita pekee huku pia ikipoteza idadi sawa ya michezo sita pia na kupata sare michezo 13  na kupelekea kujikusanyia alama 31 na kushika nafasi ya 10 katika EPL.

Arsenal pia ina uwiano mbovu wa magoli ya kufunga na kufungwa ikiwa na hasi 2 mpaka sasa ikiwa imefunga magoli 32 na kiruhusu kufungwa mabao 34 katika wavu wao.

Hali imekua tofauti kwa timu ya Mtanzania Mbwana Samatta walau wao wameonja ushindi mara nyingi zaidi ya Arsenal ambapo wamepata ushindi mara 7 katika EPL ingawa wako nafasi ya  17 wakiwa wanapigania wasishuke daraja.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.