Sambaza....

Nahodha wa Simba Sports Club John Raphael Bocco ataukosa mchezo wa klabu yake dhidi ya mahasimu wao Yanga utakaopigwa September 30.

John Bocco ataukosa mchezo huo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi baada ya kumpiga ngumi mlinzi wa klabu ya Mwadui katika mchezo uliopigwa katika dimba la Ccm Kambarage.

John Bocco alimpiga ngumi mlinzi huyo baada ya kutokea purukushani pembezoni mwa uwanja huku John Bocco akipigwa kiwiko ambacho mwamuzi hakukiona na hivyo kupelekea yeye kurudishia kwa hasira.

Licha ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi mnono wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Mwadui huku yeye akifunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza lakini alikaliza mchezo vibaya kwa kuonyeshwa kadi nyekundu ya kizembe kwa kushindwa kuzuia hasira zake.

John Bocco pia leo amekua mchezaji wa kwanza kuweza kufunga magoli 100 katika Ligi Kuu Bara, lakini ameitibua sherehe hiyo na kushindwa kusheherekea kwa kupata kadi hiyo na kupeleka kukosa michezo mitatu ya Ligi.

Sambaza....