Bocco
Blog

John Raphael Bocco Shujaa asiyepewa heshima yake.

Sambaza....

Nahodha wa klabu ya Simba sc na mchezaji wa timu ya Taifa “Taifa Stars” John Bocco “Adebayor” jana alikua mmoja ya wachezaji wa Stars waliotimiza ndoto za Watanzania zaidi ya millioni 50 kuweza kufuzu Afcon baada ya miaka 39.

Baada ya kuifunga Uganda kwa mabao matatu kwa sifuri pale Kwa Mkapa huku John Bocco akitoa pasi mbili za mabao na kuweza kua moja ya wachezaji nyota waliowasheheresha Watanzania elfu sitini waliojitokeza katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

John Bocco baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Uganda

Ndani ya siku 14 John Bocco amekua ni mchezaji mwenye bahati na furaha lakini pia kuandika rekodi katika klabu yake ya Simba sc na timu ya Taifa “Taifa Stars”. John Bocco ameweza kufuzu na Simba kuingia hatua ya robo fainali na Simba lakini pia ameweza kufuzu katika michuano ya Afcon 2019 nchini Misri.

John Bocco amekua ni mchezaji asie na habati kwa mashabiki na kushindwa kupewa heshima anayostahili kutokana na kazi anayoifanya. Amekua muhimili mkubwa kwa Klabu na timu ya Taifa katika mafanikio yote hayo.

Imekua ni nadra sana kwa John Bocco kusikika akiimbwa na mashabiki wa Stars au hata wa klabu yake huku mara nyingi wakiwa wanamlaumu na kumtupia lawama kwa kukosa nafasi za wazi. Unaweza sema watu wanachukua mabaya zaidi kuliko mazuri anayoyafanya2

John Bocco vs Al-Ahly

Katika mchezo wa jana tu John Bocco amefanikiwa kutoa “assist” mbili kwa Simon Msuva na Agrey Morris. Katika mchezo wa Simba dhidi ya Al-Ahly John pia alitoka “assist” kwa Kagere na pia kwenye mchezo wa AS Vita John pia alishirikiana na Haruna Niyonzima kupika goli la Chamma lililoivusha Simba kuelekea robo fainali.

 

John Raphael Bocco  “Adebayor” ifike wakati apewe anachostahili kutokana na mambo makubwa anayoyafanya uwanjani.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x