Sambaza....


Mwadui FC vs Stand United

Mwadui ilishinda 2-1 dhidi ya Lipuli, Stand Untd ilipoteza dhidi ya Majimaji nyumbani kwake, leo ipo ugenini.


Azam FC vs Njombe Mji

Mchezo utakuwepo kama kawaida, Chamazi Complex saa 1 jioni.


Mbao FC vs Majimaji FC

Baada ya kuwasismamisha baadhi ya wachezaji ikaibuka na ushindi mnono wa bao 3-1, je leo kufanya maajabu tena?


Azam FC vs Njombe Mji

Njombe wanahitaji kushinda mchezo huu ili kuendelea kuikimbia nafasi ya Kushuka daraja, mchezo uliopita walipoteza kwa 2-1 dhidi ya Mbao FC.

Kuna taarifa Azam FC wameomba hii mechi  isogezwe mbele, baada ya kucheza na Ruvu Shooting juzi, mechi ambayo Msemaji wa Ruvu anasema Ruvu imewapapasa Azam FC.


Lipuli FC vs Singida United

Viongozi wa klabu ya Lipuli leo wamewahamasisha mashabiki wao kufika uwanjani na kuujaza uwanja. Kauli mbiu yao ya leo wanasema “Njoo tumpe ngumi jiwe pacha na ndugu yetu Singida, Njoo tulete shangwe kuu mkoani Iringa mji wa Kitemi”


 

Sambaza....