Bocco
Ligi Kuu

Kagere: John Bocco ndie muongoza njia.

Sambaza....

Kinara wa mabao, Medie Kagere amemchambua nahodha John Bocco kuwa ni kiongozi imara ambaye siku zote anaamini katika ushindi.

Kagere ambaye anacheza sambamba na Bocco katika idara ya ushambuliaji amesema nahodha huyo siku zote mhamasishaji mkuu wa kupata alama tatu uwanjani.

Meddie Kagere na John Bocco wakiwa mbele ya Lango la Al-Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Raia huyo wa Rwanda, amesema Bocco ni mtu mpole, imara na anajua anachokifanya na amekuwa akimkubali ndani na nje ya uwanja.

Meddie Kagere “Bocco ni mtu safi, mpole na kiongozi imara na anatuongoza katika njia nzuri na wakati wote anatuhamasisha katika kutafuta ushindi uwanjani.”

John Raphael Bocco.

“Siku zote anaamini katika ushindi na ikitokea tumepoteza au kutoka sare utamuona anakosa amani na anakuja kwetu na kutupa moyo tusahau yaliyopita,” amesema Meddie Kagere ambae pia ni Galacha wa mabao mwa mwezi March kabla ya Ligi  kusimama kutokana na Corona.

Kagere anaongoza katika kufumania nyavu kwenye VPL ambapo hadi sasa ametupia mabao 19 huku mechi zikiwa zimebaki tisa kabla ya ligi kumalizika.

Chanzo: tovuti ya Simba.

Sambaza....