Uhamisho

Kiraka wa Simba atua Namungo fc.

Sambaza....

Namungo Fc yenye maskani yake Kusini mwa Tanzania mkoani Lindi imefanikiwa kumdaka mchezaji wa zamani wa  Simba na hivyo kuzidi kujiimarisha katika msimu wao wa kwanza katika Ligi Kuu Bara.

Wauaji hao wa Kusini wamefanikiwa kunasa saini ya mlinzi wa kushoto Jamal Mwambeleko akitokea klabu ya KCB ya nchini Kenya kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Jamal Mwambeleko aliposajiliwa na Singida utd akitokea Simba sc.

Jamal Mwambeleko mchezaji wa zamani wa Simba sc na Mbao mwenye uwezo wakucheza kama kiungo pia amesajiliwa na Namungo kwenda kuziba nafasi ya Paul Ngalema ambae tetesi zinasema huenda akarudi katika klabu yake ya Lipuli fc.

Kabla ya kujiunga na Namungo fc Jamal Mwambeleko ziliibuka tetesi za kua amejiunga na Bidvest Wits ya nchini Afrika Kusini huku pia akionekana katika picha akiwa katika uwanja wa timu hiyo!


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.