Zamani

Kisa cha Kalilou Fadiga kuiba cheni.

Sambaza....

Ni mapema ya mwezi juni 2002 nikikatiza kwenye viunga vya Afrikasana, jijini Dar es salaam. Taratibu naisogelea meza ya muuza magazeti huku nikimsikia mdau akisifia kwa madaha kikosi cha Senegal na kumpamba sana Kalilou Fadiga.

Binafsi sikuwahi kumtilia maanani Fadiga, kwani nyota wa kikosi hicho cha maangamizi kila mtu alikuwa anamjua, si mwingine bali ni fundi na mtukutu Al Hadji Diouf.

Siku ile niliondoka Kalilou Fadiga akiwa kichwani kwangu, nikiwa na shauku ya kumtazama kwa makini katika mechi iliyokuwa inafuata dhidi ya Denmark baada ya ile ya ufunguzi waliyomchapa 1-0 bingwa mtetezi Ufaransa. Shukrani kwa goli la marehemu Papa Bouba Diop, Mungu ampe heri huko alipo.

Nilipotazama mechi dhidi ya Denmark nikaelewa kwa nini yule jamaa alikuwa akimpamba kwa mbwembwe nyingi kiungo huyo hatari wa anayetumia guu la kushoto.

Kombe la dunia huwa halikosi vimbwanga. Moja ya vituko na tukio lililoshika vichwa vya habari ni skendo ya Fadiga kutuhumiwa kuiba cheni ya dhahabu katika duka moja la vito lililopo Taegu siku kadhaa kabla ya mechi ya ufunguzi ya Mei 31 dhidi ya Ufaransa.

Baadae mambo yalipokiwa mengi alirudisha cheni hiyo na mamlaka za Korea hazikumkuta na kesi ya uhalifu. Hivyo aliruhusiwa kuendelea na majukumu yake ya kutandaza kabumbu kwenye fainali hizo.

Stori ipo hivi! Muuza vidani kwenye duka hilo aliamua kumzawadia Fadiga kidani hicho ili kimletee bahati nzuri katika mechi atakazocheza.

Mwishowe muuza vidani huyo bwana Lee Seung-youl alijisikia vibaya kwa sababu hakutarajia skendo ingekuwa kubwa kiasi hicho. Alimuomba radhi Fadiga na maisha yakaendelea.

Fadiga akivalia uzi namba 10 aliendelea kuwa mchezaji muhimu hadi pale Senegal ilipotolewa katika hatua ya robo fainali kwa goli la dhahabu dhidi ya Uturuki.

Na Henry Hamisi
Insta@ henry_the_massive


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.