Sven Vandebroeck
Ligi Kuu

Kocha Simba: Kesho sio mchezo wa kawaida.

Sambaza....

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vadebroek amesema mchezo wa kesho sio mchezo wa kawaida kutokana na kucheza na wapinzani wao wakubwa katika Ligi huku pia akigusia pengo la alama kati yao na Yanga.

Sven ameyasema hayo alipokua akiongea na Waandishi wa habari kuelekea mchezo namba 260 wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho March 8.

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandebroek akiwa katika benchi na kocha msaidizi Selemani Matola.

Sven Vandebroek “Tunacheza mchezo huu kama sio mchezo wa Ligi sababu kila mmoja anajua  tumewaacha kwa alama kadhaa. Tutacheza kama mchezo wa kweli na wa wapinzani kwahiyo tunajiandaa kuchukua alama zote tatu na kusonga mbele ili mwisho wa msimu tushinde.”

Kocha huyo pia aligusia hali ya majeruhi katika kikosi chake  huku akisema anatarajia kuwakosa wachezaji wake wawili katika eneo la kiungo.

Said Hamis Ndemla ataukosa mchezo wa kesho dhidi ys Yanga kutokana na majeruhi.

Van Debroek ” Kwa upande wetu kila mmoja tuko fiti isipokiwa Miraji (Athumani) na Ndemla (Said) ambao ni majeruhi.  Nategemea hali nzuri kesho ambayo itaruhusu kucheza mpira na kufurahia mchezo.”

Sven anakwenda kukutana na joto la mechi ya Watani wa jadi kwa mara ya pili sasa baada ya kuwepo katika mchezo wa raundi ya kwanza ambao uliisha kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Sambaza....