
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre, kwa mujibu wa taarifa kutoka msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara.
Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.
Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi
Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.
Unaweza soma hizi pia..
Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
Kila mwanasimba anatakiwa kufahamu hilo na kukubali mambo ni magumu.
Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
Licha ya Fiston Mayele kusifiwa na kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga
George Mpole anaishi ndoto zetu!
juhudi binafsi za George Mpole na ndio maana utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa ni 1 kwao lakini yeye pekeake Mpole ana mabao 13.
Alli Kamwe: Kumbe bila moto wanateseka!
: Asante Moalin. Asante Pablo Franco, Mechi ilichezwa sana kwenye mbinu kisha ikamalizikia kwenye Ufundi wa wachezaji.