Nasraddine Nabi akiwa na mashabiki wa Yanga.
Shirikisho Afrika

Kocha Yanga:Tunapenda Kucheza Mbele ya Mashabiki Wengi

Sambaza....

Yanga wanashuka dimbani kesho jioni kumenyana na Marummo Gallants katika mchezo wapili wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kocha wake Nasradine Nabi amesema wapo tayari kucheza mbele ya mashabiki wengi wa timu pinzani.

Tayari Yanga wana uongozi wa mabao mawili walioupata katika mchezo wa awali na wenyeji tayari wamesema mchezo huo utakua hakuna kiingilio mashabiki wote wataingia bure katika mchezo huo. Kuelekea mchezo huo amesema
“Tumesahau kuhusu faida ya ushindi wa 2-0 tulioupata kwenye uwanja wa nyumbani. Huu ni mchezo mwingine na tuko na mpango mwingine wa dakika 90 za hapa.”

“Ni jambo zuri Marumo wamepanga mechi isiwe na kiingilio. Sisi kama Yanga tunapenda kucheza mbele ya mashabiki wengi kuliko uwanja kukosa mashabiki. Nina wachezaji wenye uzoefu wa kutosha wa kucheza mechi za namna hii,” alisema Nabi

Nae Kenedy Musonda akiongea kwa niaba ya wachezajo wenzake amesema wamejiandaa vyema na wanatarajia kurudi nyumbani wakiwa washindi. 

Kennedy Musonda “Maandalizi ni mazuri sana kwa upande wetu wachezaji na tunajua tumekuja kwenye mchezo mkubwa. Tuko tayari kupambana na kurudi nyumbani tukiwa washindi.” 

Sambaza....