Ligi Kuu

Kwa hili la Makambo tunaelekea kuzuri!

Sambaza....

Baada ya mshambuliaji tegemeo wa Yanga Mcongomani Heritier Makambo kuonekana akiwa amesainiwa na klabu kutoka Guinea maneno mengi yameibuka kuhusu uhalali huo wa yeye kusaijiliwa angali bado mchezaji wa Yanga.

Bado ni kizungumkuti kutokana na usajili huo wa Makambo huku akielekea Guinea akiwa na kocha wake Mcongo mwenzie Mwinyi Zahera. Bado haijulikani rasmi kama pesa aliyosajiliwa Heritier Makambo ni mali ya Yanga sc alipo sasa au ni ya DC Motema Pembe ambako inasemakana walimtoa Yanga acheze kwa mkopo.

Yote kwa yote ni Yanga wenyewe ndio wanaojua ukweli katika hili.

Makambo akikabidhiwa zawadi yake baada ya kua GALACHA wa mabao kwa mwezi November na msimamizi wa tovuti ya kandanda, Thomas Mselemu.

Ukitazama kwa mtazamo chanya baada ya usajili wa Heritier Makambo kutoka Yanga sc kwenda Horoya ya Guinea utaona Ligi Kuu Bara (TPL) imetoa tena mchezaji na kusajiliwa nje ya nchi.

Ukiachana na Yanga kufaidika ama kutokufaidika na mauzo ya Makambo tayari nchi imefaidika na mauzo yake kutokana na kuzidi kuitangaza Nchi na Ligi yetu huko aendako. Hii inaonyesha  pia ukuaji wa Ligi yetu.

Shiza Kichuya amejiunga na ENPPI akitokea Simba sc

Kwa msimu huu tuu tayari Ligi yetu imetoa zaidi ya wachezaji watatu waliokwenda katika nchi zilizoendelea kisoka na hivyo kuongeza thamani ya Ligi yetu na kufanya izidi kufwatiliwa na mawakala zaidi.

Kabla ya Heritier Makambo kwenda Horoya fc (Ilishiriki hatua ya makundi katika klabu bingwa Africa) tayari Ligi yetu ilishatoa wachezaji kama Yahya Zayd, Kichuya na Ambokile kwenda kujiunga na vilabu vilivyopo nchi zilizoendelea kisoka.

Eliud Ambokile amejiunga na Leopard ya Africa Kusini akitokea Mbeya City

Yahya Zaid(Ismailia-Misri), Shiza Kichuya (ENNPI- Misri), Eliud Ambokile (Black Leopards-Afrika Kusini) wachezaji wote hawa waliondoka Tanzania katika dirisha dogo. Hivyo bado tuna nafasi ya kutoa wachezaji wengine katika usajili wa dirisha kubwa.

Kwa kuendelea kutoa wachezaji kutoka moja kwa moja kwenye Ligi yetu (TPL) na kusajiliwa na vilabu vya nchi zilizoendelea kisoka tena bila kufanyiwa majaribio iaonyesha ni jinsi gani nchini yetu tunapiga hatua kisoka.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.