Lipuli fc
Ligi Kuu

Lipuli fc kama ilivyotarajiwa!

Sambaza....

“Wanapaluhengo” wajukuu wa Mkwawa wamejikuta wakipoteza mchezo mbele ya Wekundu wa Msimbazi katika uwanja wao wa nyumbani wa Samora kama ambavyo ilivyotegemewa na mashabiki wa mpira.

Kutokana na hali mbaya ya kiuchumi huku pia ikimkosa mshambuliaji wao kiongozi Paul Nonga “Baba Jackiee” Lipuli fc aliekwenda kufanya majaribio nje ya nchi imekubali kichapo cha bao moja kwa sifuri mbele ya Simba katika mchezo wa raundi ya 22 ya Ligi Kuu Bara.

Bao pekee la Simba lilifungwa na nahodha John Bocco katika dakika ya 23 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Francis Kahata  Nyambura ambae anafikisha “asisst” ya sita msimu huu katika VPL.

Nahodha  John Bocco akishangilia goli baada ya kuifunga Lipuli fc.

Kwa matokeo hayo Lipuli inabaki na alama zake 29 huku ikiwa na imecheza michezo 22 mpaka sasa huku ikishika nafasi ya 11 katika msimamo.

Simba wao wanaendelea kujichimbia kileleni wakiwa na alama 56 wakifwatiwa kwa mbaali na Azam fc wenye alama 44 katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.