ASFC

Manara: Mashabiki hawatotuelewaa!

Sambaza....

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara ameweka wazi kuwa mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga SC wanahitaji ushindi ili kutunza heshima ya klabu.

Manara amezungumza na tovuti rasmi ya klabu na kusema baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa ligi kwa mara ya tatu mfululizo furaha itakuwa maradufu kama watafanikiwa kuwatoa Yanga na kuingia fainali ya FA siku ya Jumapili.

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Masingisa akiwa na msemaji wa Simba Hajji Manara

Hajji Manara “Baada ya kupoteza mchezo uliopita tuliopokutana haitaleta picha nzuri mbele ya mashabiki wetu kama hatutapata ushindi na kutolewa.

Kuhusu hali ya wachezaji hilo msitie shaka wako na wameupa umuhimu mkubwa mchezo huu.”

Benard Morisson.

Simba inakwenda kukutana na Yanga kwa mara ya tatu msimu huu huku ikiwa imeambulia sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wa kwanza huku wapili wakifungwa bao moja bila lililofungwa na Benard Morisson.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.