Ligi Kuu

Masau Bwire: Mayele alikua anahangaika uwanjani!

Sambaza....

Mchezo kati ya Ruvu Shooting na Yanga umemalizika kwa suluhu katika dimba la Lake Tanganyika Kigoma. Licha ya safu ya ushambuliaji ya Yanga kuogozwa na Fiston Mayele lakini haikuambulia chochote mbele ya walinzi wa Ruvu Shooting.

Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire alimzungumzia mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele baada ya kushindwa kufunga bao katika mchezo huo ulioisha kwa suluhu mkoani Kigoma.

Fiston Mayele alithibitiwa na mlinzi wa Ruvu Shooting.

“Miongoni mwa wawakilishi wetu Kimataifa huko ni hawa, mmeona walivyopata tabu leo mbele ya Ruvu Shooting.,” Masau Bwire alisema

“Mayele mliesema anatetema nilisema atatetemeka kwa hofu na mashaka na ndicho kilichotokea uwanjani.
Mayele alikua anahangaika kama muuza migebuka soko la Kigoma, alikosa kabisa maarifa ya kuipenya ngome ya Ruvu Shooting.” Masau Bwire


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.