Ligi Kuu

Mashabiki Simba bado wana imani na timu yao!

Sambaza....

Licha ya msimu 2021/22 kutokuwa mzuri kwa upande wa klabu ya Simba baada ya kushindwa kutetea vikombe vyote viwili walivyobeba msimu uliopita lakini bado mashabiki  wao  wanaimani na furaha na timu hiyo.

Mashabiki hao bado wamejitokeza katika mchezo wa mwisho wa kumuaga mlinzi wao wa kati Pascal Wawa raia wa Ivory Coast ambae msimu huu utakuwa msimu wake wa mwisho kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi Simba.

Mashabiki wa Simba wakiwa wameshika mataji na kapu wakifurahia ushindi dhidi ya Mtibwa (picha na Catherine Mbaga).

Baada ya mchezo huo kumalizika mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo walilizunguka gari lililobeba wachezaji  wakiwashukuru kwa juhudi walizozionyesha msimu huu licha ya kuambulia kombe la Mapinduzi pekee.

Rasmi sasa Simba wamemaliza michezo yao ya nyumbani na wamebakiza mechi mbili ugenini dhidi ya Mbeya Kwanza Majimaji Songea na Tanzania Prison Sokoine Mbeya ili kukamilisha msimu 2021/22!


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.