Baada ya kufunguliwa kwa usajili wa dirisha dogo barani Ulaya vilabu mbalimbali vimekua busy kutafuta wachezaji watakowasajili ili kuongezea nguvu katika vikosi vyao. Dirisha dogo majira ya baridi limefunguliwa tangu January mosi na litafungwa January 31.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” amekua akigonga vichwa vya habari katika magazeti na mitandao mbalimbali Ulaya na hapa nchini kutokana na kutakiwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya.
Klabu ya soka ya Cardiff iliyopo EPL imeonyesha nia ya kumuhitaji mshambuliaji wa KRC Genk Mbwana Samata ili akiongezwe nguvu kikosi hicho kinachopambana ili kisishuke daraja. Cardiful inashika nafasi ya 17 huku ikiwa na alama 19.
Kwa mujibu wa gazeti la Dailymail Cardiff imetuma maombi kwa KRC Genk ili kumpata mshambuliaji huyo anaeongoza kwa mabao mpaka sasa katika Jupiter pro League ya nchini Ubelgiji akiwa na mabao 15 huku ikiiwezesha Genk kuongoza ligi ikiwa na alama 48 kileleni.
Bado haijatajwa wametuma ofa kiasi gani ili kumng’oa nahodha huyo wa Stars katika klabu yake ya sasa ili kumuhamishiaa kwenye ligi ya Kibabe ya EPL.