Sambaza....

Leo ligi mbalimbali zinaendelea, tumekuletea mechi tano ambazo zinaweza zikakusaidia upate mpunga wako.

LIVERPOOL vs CRYSTAL PALACE.

LIVERPOOL KUSHINDA.

Sababu:

Katika mechi tano zilizopita Liverpool kashinda mechi 3 na akafungwa mechi 2 , huku Crystal Palace katika mechi 5 zilizopita ameshinda mechi 2 akapoteza mechi mbili na akatoka sare mchezo mmoja, kwa hiyo Liverpool anamatokeo mazuri ya mechi za hivi karibuni kuzidi Crystal Palace.

Klop (Kocha wa Liverpool)

Liverpool hajafungwa katika mechi 31 zilizopita na timu yoyote katika uwanja wake wa nyumbani. Kwa hiyo ana matokeo mazuri kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Liverpool hajafungwa zaidi ya magoli 2 katika mechi 16 zilizopita huku akifanikiwa kupata clean sheets mechi 12 kwenye hizo mechi 16 zilizopita na kuruhusu goli 4 tu kwenye hizo mechi 16 zilizopita.

MANCHESTER UNITED vs BRIGHTON.

MANCHESTER UNITED KUSHINDA.

SABABU:

Manchester United ameshinda mechi tano zilizopita , huku Brighton kwenye mechi tano zilizopita ameshinda mbili, akatoka sare mchezo mmoja na kufungwa mchezo mmoja. Kwa hiyo Manchester United amekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za hivi karibuni kuzidi Brighton.

Manchester United haijawahi kufungwa na Brighton kwenye mashindano yote kwenye uwanja wa nyumbañi wa Manchester United (Old Trafford), huku Manchester United akishinda mara 4 mfululizo dhidi ya Brighton kwenye uwanja wake wa nyumbani. Kwa hiyo Manchester United ana matokeo mazuri dhidi ya Brighton katika uwanja wake wa nyumbani.

Mara ya mwisho kwa kocha wa Brighton, Chris Hughton kushinda ugenini dhidi ya “TOP SIX” ilikuwa msimu wa mwaka 2012/2013 , amepoteza mechi 14 za ugenini dhidi ya “TOP SIX”. Hivo kocha wa Brighton ana matokeo mabaya dhidi ya ” TOP SIX” Kwenye viwanja vya ugenini.

ARSENAL vs CHELSEA

TIMU ZOTE KUFUNGANA / SARE.

SABABU

Kwenye mechi 5 zilizopita, Arsenal kashinda mechi 2, akapoteza mechi 2 na akatoka sare mechi 1. Wakati Chelsea katika mechi tano zilizopita kashinda mechi 3, akatoka sare mchezo mmoja na kufungwa mchezo mmoja. Hapa unaona timu zote zinamatokeo yenye picha inayokaribiana katika mechi za hivi karibuni.

Unai (Kocha wa ARSENAL)

Kwanini watafungana ?, Arsenal Kwenye mechi 5 zilizopita amepata clean sheet moja tu. Hii inaonesha ukuta wake ni dhaifu, huku akiwa amefunga magoli 13 na kufungwa magoli 4 Kwenye mechi tano zilizopita.

Wakati Chelsea katika mechi zilizopita amefungwa magoli 2 na kufunga magoli 5. Chelsea inakutana na timu ambayo ina safu mbovu ya ulinzi na safu bora ya ushambuliaji ambapo Kwenye mechi 5 zilizopita Arsenal imefunga magoli 13 wastani wa kufunga goli 2.5 Kwenye kila mechi, kwa hiyo Arsenal inatabia ya kuruhusu magoli na kufunga magoli.

PSG vs GUINGAMP

PSG KUSHINDA

SABABU

PSG anashika nafasi ya 1 Kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ufaransa (Ligue One) , wakati Guingamp anashika nafasi ya mwisho Kwenye msimamo. Hii inaonesha PSG ni bora zaidi ya Guingamp.

Neymar, Mchezaji wa PSG

Katika mechi 14 ambazo ziliwakutanisha PSG na Guingamp, PSG ameshinda mechi 9 wakatoka sare michezo miwili na Guingamp akashinda michezo 3. Kwa hiyo PSG ana matokeo mazuri ya hivi karibuni dhidi ya Guingamp.

RB LEIPZIG vs BORRUSIA DORTMUND.

TIMU ZOTE KUFUNGANA.

KWANINI

Ukiangalia katika mechi tano zilizopita, Rb Leipzig amefunga magoli 9 na kufungwa magoli 4 na Borrusia Dortmund akiwa amefunga magoli 11 na kufungwa magoli 7.

Timu zote zinawastani wa kufungwa Kwenye kila mechi angalau goli moja, pia zina wastani wa kufunga goli angalau mechi moja. Kwa hiyo zinakutana timu ambazo zinafunga na safu zao za ulinzi zinaruhusu magoli.

Sambaza....