Luis Miquisone
Tetesi

Miquissone Aigomea Al Ahly, Azam Fc Yavamia Al Hilal

Sambaza....

Mabosi wa Azam FC imefikia sehemu nzuri juu ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Al Hilal, Lamin Jarjou ili kujiunga nao katika unaotarajiwa kufungulia mwanzoni mwa Julai. [Mwanaspoti]

Fred Felix Minziro ameachana na klabu ya Geita Gold aliyodumu nayo tangu daraja la kwanza. Namungo Fc, Mbeya City na Tabora Utd (Kitayosce) zimeonyesha nia ya kumuhitaji nyota huyo wa zamani wa Yanga. [Mwanaspoti]

Erasto Nyoni amejiunga na Namungo Fc baada ya kuachana na Simba aliyodumu nayo takribani miaka sita. Erasto anakwenda kuungana na Namungo na kuifanya kuwa klabu ya tatu kuitumikia hapa nchini baada ya Azam Fc na Simba.

Yahya Mbegu.

Klabu ya Cotton Sports ya Cameroon imekataa ofa iliyotumwa na Simba wakimtaka mlinzi wa kati Che Fonde Malone. Nyota huyo yupo tayari kuachana na tim hiyo ili ajiunge na Simba huku pia akiwa ameshakataa kuongeza mkataba na Wacameroon hao [Nuhu Adam]

Mlinzi wa kushoto Yahya Mbegu ameshamalizana na Simba baada ya mkataba wake kumalizika Ihefu, Mbegu pia alikua anawaniwa na Singida Fointaine Gate lakini kila kitu kwa Simba tayari na anasasubiri kutambulishwa tu [Champion]

Yanga ipo tayari kumbakisha Fiston Mayele wakimuwekea dau kubwa la dola 500,000 na mshahari wa dola 12,000ili aweze kusaini mkataba wa miaka mitatu na kuzidhibiti timu zinazomtaka nyota huyo wa Congo [Champion]

Andre Onana.

Klabu ya Manchester imepiga hatua zaidi katika harakati za kuinasa saini ya mlinda mlango wa Inter Milan Andre Onana ambae anahusishwa pia na klabu ya  Chelsea[Dan Shelgon]

Winga Luis Miquissone amesema anahitaji kupata suluhisho la kudumu dhidi ya klabu yake ya Al Ahly. Luis ambae anahusishwa na kurejea Simba anataka kuondoka Al Ahly jumla na si kumtoa kwa mkopo [Kick off]

Mshambulizi wa Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 30, anavutiwa na Lazio huku kandarasi yake ikitarajiwa kumalizika mwezi huu [Sky Sports Italia]

 

 

Sambaza....