Uhamisho

Mo Dewji: Simba haitosajili.

Sambaza....

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na muwekezaji wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji leo amefichua mipango ya klabu ya Simba katika dirisha kubwa la usajili lililofunguliwa August 1.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mo Dewji amesema klabu yao haitofanya usajili mkubwa kipindi hiki kama ambavyo mashabiki wengi wanavyosubiria.

Kupitia ukurasa wake Mo ameandika “Timu nzuri hazisajili sana!”

 

Baada ya klabu ya Yanga kuanza vurugu za usajili na Azam fc mashabiki wengi wa Simba wamekua wakisubiri kwa hamu kuona maboss wa Msimbazi wakijibu mapigo kwa kutambulisha nyota wapya watakaoingia kikosini.

Simba kupitia CEO wake Senzo tayari walishasema huenda wakasajili wachezaji watano tu miongoni mwao wapo wa ndani ya nchi na Kimataifa. Tetesi zilizopo mpaka sasa Simba imeshamalizana na Kameta Duchu (Kutoka Lipuli fc) na Charles Ilanfia (KMC) huku wakizidiwa kete na Yanga kwa mlinzi Bakari Mwamunyeto.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.