Ligi Kuu

Mo: Namtakia kila la kheri Senzo

Sambaza....

Baada ya aliekua CEO wa klabu ya Simba kujiuzulu na kutimkia upande wa pili na kuibukia klabu ya Yanga Mwenyekiti wa klabu ya Simba amesema anamtakia kila lakheri katika timu yake mpya huko alipo.

Mwekezaji huyo wa klabu ya Simba amesema Simba itapata mtu mwingine makini zaidi na Simba haiwezi kutetereka maana ni taasisi kubwa kuliko mtu mmoja.

Mohamed Dewji ” Namtakia kila lakheri Senzo katika timu yake mpya na majukumu yake mapya huko alipo. Pia nawatakia kila lakheri upande wa pili katika usajili wao unaoendelea.

Niwahakikishie wana Simba ni taasisi kubwa  kuliko mtu yoyote. Tutapata Mtendaji mwingine mzuri zaidi na shughuli zitaendelea kama kawaida”

Mo pia alizungumzia uwezo wa Larry Bwalya na kumwagia sifa huku akijinasibu ni mchezaji mzuri sana kwa mujibu wa ripoti mbalimbali walizozipata kwa makocha wa Zambia na watu wa karibu.

Larry Bwalya

Mo “Kama huyu Rally Bwalya ni mchezaji mzuri sana tumepata taarifa  zake, mtu kama Micho ni kocha mkubwa baada ya kutoka Yanga alikwenda mpaka Zamalek huko ambako alikua analipwa dola 25 mpaka elfu 30, lakini ametuhakikishia Bwalya ni mchezaji mzuri.

Wachezaji kama hawa wenye umri mdogo na wenye uwezo ndio maana tuwasajili kwa zaidi ya miaka miwili.”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.