David Molinga "Falcao"
Ligi Kuu

Molinga amuanzishia vita kimyakimya Kagere

Sambaza....

Ligi Kuu Bara inashika kasi huku vita ya kuwania ubingwa na ipe ya kushuka daraja ikiwa inazidi kushika kasi na upande wa pili huku kuna vita ya kuwania  ufungaji bora nayo ikiwa yamoto.

Mpaka sasa katika kuwania Galacha wa magoli wa VPL ni Meddie Kagere ndie yupo kileleni akiwa na mabao 15 akiendelea kujiimarisha kileleni baada ya jana kuongeza goli katika mchezo dhidi ya Azam fc.

David Molinga ameonekana kutokua nyuma katika vita hii huku  akianza kujitutumua na kwa mara ya kwanza msimu huu Molinga ameingia Top 4 ya ufungaji magoli. Mpaka sasa Molinga ana mabao nane huku  akiwa anashika nafasi ya nne akiwa nyuma ya Kagere (mabao 15), Mhilu  (11), Lusajo (10),

Baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati katika mchezo dhidi ya Alliance sasa David Molinga anafikisha mabao 8 na hivyo kuanza kumkimbiza kinara Meddie Kagere aliepo kileleni. Kwa kasi ya Molinga ni wazi sasa vita ya ufungaji inazidi kua tamu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.