
Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani katika moja ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika
Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Alli amekiri msimu huu ni ngumu wao kutwaa ubingwa kutokana na aina ya matokeo wanayoyapata katika Ligi.
Ahmed Ally amekiri mambo ni magumu na kitendo cha kutoka sare dhidi ya Azam kinazidi kuwapa wakati mgumu na kuwapa faida Yanga.
“Tunaendelea kumpa faida mpinzani wetu na asilimia kubwa zipo kwake, tunaendelea kupambana lakini mambo ni magumu na kila Mwanasimba anatakiwa kuelewa hivyo kwasasa.” Ahmed Ally.

Mpaka sasa Yanga wapo kileleni wakiongoza Ligi kwa tofauti ya alama 10, wakiwa na alama 60 wakati Simba wana alama 50 nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kituo kinachofwata kwa Simba ni Mwanza katika dimba la CCM Kirumba katika mchezo dhidi ya Geita Gold.
Unaweza soma hizi pia..
Mtibwa na mchezo wao wa karata.
Kama ningeulizwa ya Mtibwa Sugar FC ilipaswa kuwa timu ya mchezo gani basi jibu langu la moja kwa moja ingekuwa...
Ilikua ni Sopu dhidi yaYanga.
Sopu alivunjavunja ile 'partnership ' ya Job na Mwamnyeto ya ndani ya klabu na timu ya Taifa, maana huwa wanacheza hivyo hivyo
Mpole ni sugu aliahidi ufungaji bora!
ni sugu na jasiri sana hana uwoga hata kidogo na ni mtu wa kujitoa mhanga na ni mpambanaji haswa.
Yanga yataja siku ya kumtambulisha Aziz Ki!
Senzo Mazingisa pia alikanusha uvumi wa Fiston Mayele kusajiliwa na Kaizer Chiefs na kusema kuna wanahabari wanataka kuwachanganya.